Friday, January 5, 2018

MAFYOKSI - MATUNDA YA LUSHOTO


MAFYOKSI (kwa wasambaa) yanajulikana pia kama Crab apple au Plums peaches kwa lugha ya kiingereza.
Haya ni matunda yanayopatikana kwa wingi sana Lushoto, kwa radha ni matamu sana kwa mlaji, yanafanana sana (kwa karibu) kiumbo, radha, kokwa, mti na msimu na Matunda Damu (plums) au Faume - Kisambaa).

Fyoksi [Peach (Prunus persica)] ni tunda la mti wenye asili ya eneo la Kaskazini Magharibi mwa China kati ya Bonde la Tarim na mteremko wa kaskazini wa milima ya Kunlun Shan, ambapo miti ya matunda haya  ilikuwa ya kwanza kuzalishwa na kukuzwa.

Ukiwa Lushoto, matunda haya utayapata kwa wingi miezi ya septemba (mwishoni mwa mwaka) hadi mwishoni mwa mwezi januari (mwaka unaofuata).

Miti ya Fyoksi huwa si mikubwa kama ya miembe au parachichi, bali huwa katika kimo cha chini na si imara kwa mvunaji kuweza kuikwea/ kupanda juu na kuvuna matunda, kwani huweza kuinama ama kuvunjika.

Miti hii ya Fyoksi inazaa matunda ambayo huitwa Fyoksi.

Miti wenyewe huweza kuvumilia joto kwa karibu -26 hadi -30 ° C (-15 hadi -22 ° F), ingawa msimu wa maua ya vitunda  mara nyingi  hufa katika kipindi hicho ili  kuzuia/kuulinda  mmea huu wakati wa majira ya joto.

Kufa kwa maua ya vitunda vya Fyoksi huanza kutokea kati ya -15 na -25 ° C (5 na -13 ° F) jotoridi, kulingana na mkulima/ kilimo na wakati wa baridi, na vitunda vya Fyoksi kuwa chini ya uvumilivu baridi mwishoni mwa msimu wa baridi kali (kipupwe).

Kilimo cha miti ya Fyoksi kwa kawaida kinaanza kuzaa matunda katika mwaka wao wa tatu tangu kupandwa na kukuzwa vizuri.
Fyoksi ni matunda yanayopatikana kwaraisi, na kwa kipindi cha msimu wake, huwa yanapatikana nyumbani, mashambani, katika vichaka, ama kuuzwa sokoni.

0 comments:

Post a Comment