Lushoto view

LUSHOTO RISE-UP ....lets create its future.

Lushoto view

LUSHOTO RISE-UP ....lets create its future.

Lushoto view

LUSHOTO RISE-UP ....lets create its future.

Lushoto view

LUSHOTO RISE-UP ....lets create its future.

Lushoto view

LUSHOTO RISE-UP ....lets create its future.

Saturday, October 24, 2015

BURUDANI NI SEHEMU YA MAISHA YETU

BURUDANI NI SEHEMU YA MAISHA YETU . . . . TUWAPO KIJAMII ZAIDI VIPO VIKUNDI VINGI VYA SANAA KAMA VILE NYIMBO, MASHAIRI, NGOMA, MAIGIZO, NA KADHA WA KADHA ..........KARIBU LUSHOTO.


=>>>>> MAGHUNDAA ( matarumbeta)

=>>>>> HIZI NGOMAA ZABHUUDISHAA JAMII ZHOSHEEE ngoma hizi zaburudisha jamii yote ) . . . .  SOI NYOSHEE MSHEEZIGHE njooni nyote mcheze ). . . !!!!

JITENGENEZEE BUSTANI NDOGO NA YA GHARAMA NDOGO NYUMBANI


Zipo namna anuai za kukuwezesha kujipatia mboga nzuri, safi, bora na salama kwa afya yako. Unaweza kujihakikishia mboga salama isiyotumia kemikali na itakayokughalimu kiasi kidogo cha pesa na muda kidogo. Aidha, kulinda mboga zako dhidi ya magonjwa na vijidudu katika upandaji, ukuzaji na mavuno. 

Kuna aina nyingi za bustani ndogo unazoweza kujitengenezea nyumbani na ambazo huitaji kuwa na eneo kubwa la ardhi. Kwa mfano, unaweza kutumia ndoo/makopo amabayo mara nyingi hunayatumia kupanda maua kando ya nyumba yako, au unaweza tumia gunia la kubwa kama “kiloba au mfuko wa plastiki “Rambo”” ama unaweza tengeneza key hole garden (bustani ya tundu la Ufunguo)


MFANO HII BUSTANI YA NDOO/MAKOPO HUWAJE?
Kwanza kuwa na udongo, makopo/ndoo, mchanga au Pumba za mpunga, Mbole ya samadi iliooza vizuri. Udongo ni kwaajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea, mchanga husaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa; na mbolea ya samadi huongeza virutubisho kwa mmea. 

Sasa changanya udongo wako na mchanga pamoja na mbole katika uwiano wa 5:2:1.( yaani 5 udongo, 2 samadi, 1 Mchanga) kisha toboa makopo/ndoo yako kwa chini ili kuzuia maji kubaki kwa wingi kwenye kupo na weka pamba/sponji kwenye matundu uliotoboa. Hapo utakuwa tayari kupanda mbegu zako ama mche wa mboga aina yoyote.
=>>>> http://www.bhg.com/gardening/vegetable/vegetables/growing-vegetables-in-containers/

Mboga yoyote utakayopanda katika ndoo zako, utalazimika kumwagilia mara baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga. Ila unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku. Mboga kama sukuma-wiki,nyanya,chainizi na bilinganya waweza kuvuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu. Aidha unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda (baada ya mavuno mawili) ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.

Friday, October 23, 2015

KILIMO NA UKUZAJI WA ZAO # NYANYA

Nyanya ni aina ya mboga inayo zalishwa kwa wingi sana duniani. Kwa wilaya ya # LUSHOTO, nyanya ni zao la kipaumbele katika mazao ya mboga linalo limwa na kuliwa kwa wingi ukilinganisha na mboga zingine. Nyanya hutumika karibu Katika kila mlo. Kulingana na umuhimu wa zao hili kama chakula na pia kama zao linalomwingizia kipato Mkulima, kuna haja ya kutoa mafunzo kuhusu mbinu bora za uzalishaji wake. Pia kuna umuhimu wa kuelekeza wakulima wa lushoto na wakulima tarajali kutoka sehemu zingine wasiolima zao hili ili nao waweze kuzalisha nyanya na hivyo kuongeza idadi ya aina za mboga katika maeneo yao ili kujiongezea kipato na uhakika wa mboga. JIFUNZE !!!!!!