Zipo namna anuai za kukuwezesha kujipatia mboga nzuri, safi, bora na salama kwa afya yako. Unaweza kujihakikishia mboga salama isiyotumia kemikali na itakayokughalimu kiasi kidogo cha pesa na muda kidogo. Aidha, kulinda mboga zako dhidi ya magonjwa na vijidudu katika upandaji, ukuzaji na mavuno.
Kuna aina nyingi za bustani ndogo unazoweza kujitengenezea nyumbani na ambazo huitaji kuwa na eneo kubwa la ardhi. Kwa mfano, unaweza kutumia ndoo/makopo amabayo mara nyingi hunayatumia kupanda maua kando ya nyumba yako, au unaweza tumia gunia la kubwa kama “kiloba au mfuko wa plastiki “Rambo”” ama unaweza tengeneza key hole garden (bustani ya tundu la Ufunguo)
MFANO HII BUSTANI YA NDOO/MAKOPO HUWAJE?
Kwanza kuwa na udongo, makopo/ndoo, mchanga au Pumba za mpunga, Mbole ya samadi iliooza vizuri. Udongo ni kwaajili ya kuwezesha mmea kusimama, pia kupatia virutubisho mmea, mchanga husaidia mizizi kupita kwa urahisi, pia kuweka mazingira mazuri ya hewa na maji katika udongo yaani mzunguko wa maji na hewa; na mbolea ya samadi huongeza virutubisho kwa mmea.
Mboga yoyote utakayopanda katika ndoo zako, utalazimika kumwagilia mara baada tu ya kupanda na kuendelea ikitegemeana ni aina gani ya mboga. Ila unapoona magonjwa hasa fangasi wa ukungu na wadudu wa mboga unaweza tumia dawa zisizo za kikemikali za viwandani kama vile majani ya pilipili kichaa, mwarobaini na tumbaku. Mboga kama sukuma-wiki,nyanya,chainizi na bilinganya waweza kuvuna mara kwa mara, kazi yako ni kumwagilia tu. Aidha unatakiwa kubadilisha udongo wako kwa muda (baada ya mavuno mawili) ili kuakikisha mboga zako zina pata virutubisho ya kutosha.