Saturday, November 7, 2015

UTAMU WA LUGHA YA KISWAHILI

Kiswahili ni lugha ya Kibantu yenye misamiati mingi ya Kiarabu (karibu asilimia thelathini), lakini sasa ya Kiingereza pia (karibu asilimia kumi), inayozungumzwa katika eneo kubwa la Afrika ya Mashariki (katika nchi za Kenya, Tanzania, Uganda, Burundi na Rwanda).

Lugha hii ina utajiri mkubwa wa misamiati, misemo, methali, mashairi, mafumbo, vitendawili na nyimbo. Kiswahili hutumika kufundishia shuleni na kuna vitabu vingi vilivyotungwa kwa kutumia lugha hiyo, vikiwa pamoja na vile vya hadithi, hekaya au riwaya.
Lugha iwayo yote ina maendeleo yake aidha inaweza kukua, kukwama au kufa. Athira nyingi hutokea bila mpangilio pale ambako wasemaji wanapokea maneno mapya, wanaacha kutumia maneno mengine au hubadilisha kawaida ya matamshi au sarufi. Haya yote hutokea pia katika uwanja wa Kiswahili.

Kuna mzaha unaosimuliwa hasa Tanzania: Kiswahili kilizaliwa Unguja, kilikua Tanzania Bara, kikafa Kenya na kuzikwa Uganda.
.......... ha ha haaaa  aaah......... 
Hali halisi Kiswahili kina maendeleo yake katika nchi hizo zote labda zaidi Kongo.


Lakini itategemea pia juhudi za serikali kama umoja wa lugha utatunzwa kwa sababu kuna athari nyingi kutoka lugha za kila eneo zinazoingia katika ukuzi wa Kiswahili kwa namna zinazotofauitiana.


Embu tazama mifano hii kadhaa ya ukuaji wa msamiati wa kiswahili toka katika misamiati ya lugha ya kiingereza.............


Password - Nywila.
Juice - sharubati.
Chips - vibanzi.
PhD - uzamifu.
Masters - uzamili.
Degree - shahada.
Diploma - stashahada.
Certificate - Astashahada.
Keyboard - kicharazio.
Scanner - mdaki.
Flash disk - diski mweko.
Mouse - kiteuzi.
Floppy disk - diski tepetevu.
Computer virus - mtaliga.
Distillation- ukenekaji.
Evaporation - mvukizo.
Synthesis- uoanishaji.
Oesphagus- umio.
Green house - kivungulio.
Femur - fupaja.
Germ cell - selizazi.
Humus - mboji.
Nector - mbochi.
Nector - Ntwe.
Nutrients - virutubisho.
Appetizers - vihamuzi.
ATM - Kiotomotela.
Bussiness card - kadikazi.
Scratch card - kadihela.
Simcard - kadiwia/mkamimo.
Memory card - kadi sakima.
Micro wave - Tanuri ya miale.
Laptop - kipakatarishi.
Power saw - msumeno oto.
Duplicating machine - kirudufu.
Photocopier- kinukuzi.
Cocktail party - Tafrija mchapulo.
Air conditioner- Kiyoyozi.
Lift- kambarau

 Sasa kazi kubwa ni pale utakapolazimika kutumia misamiati hiyo katika mazungumzo ya kawaida...............sijui kama utaeleweka kirahisi......
''Baada ya kusahau nywila (password) ya kadi yangu ya  kiotomotela(ATM) nikaamua kukaa mgahawani (restaurant) jirani na kilipo  kiotomotela na kuagiza vibanzi (chips) vikavu na sharubati (juice) baridi sana!

Nikiwa nasubiri kuletewa nikafungua kipakatalishi (laptop) changu na kujaribu kufungua diski mweku (local disk) iliyogoma kufunguka kwa wakati huo. Nikafungua diski tepetevu (floppy/hard disk) na kukuta imevamiwa na mtaliga(virus), nguvu ikaniishia nikashindwa hata kushika wala kupalaza kisharazio(cursor). Siku yangu ikaishia hapo na nikaishia kusahau hata vibanzi na sharubati nilivyoagiza.''


.....duuuuuuh...........


#KISWAHILI . . .  shikamoo !!!!!!!

0 comments:

Post a Comment