Wednesday, September 20, 2017

MWONEKANO WA MIJI YA KASIGA, MAZINDE NA MAZINGE NGUA TOKA KILELE CHA SHULE YA MSINGI MHELO

  
Uwapo katika matembezi . . .  fika na tembelea shule ya msingi mhelo. Hapo utafurahi na kuburudisha macho na kustarehesha fikra zako; pengine ukawa na mawazo chanya yasiyo na uzimbezimbe👌
Katika shule hiyo, upande wa kushoto mwa majengo ya shule, ndiko kwenye ukanda ama ukingo (uitwao mwisho wa ardhi) ambapo ukisimama na kutazama bonde lenye kina cha urefu unaoshangaza, kuogofya ama kuburudisha . . .  utapata kujionea maeneo mbalimbali ya miji ya Kasiga, Mazinde, Mazinde ngua na mingine mingi sanjari na barabara kuu ya Dar es Salaam - Arusha.


Kwa kweli hii ni sehemu maridhawa sana, ambapo utapata kushuhudia vitu mbalimbali vikiwa katika maumbo ya udogo. Mfano kama nyumba na magari yapitayo, hupata kuonekana mithili ya vitu vidogo sana kutokana na umbali ulioko kati ya vitu hivyo na mahali alipo mtazamaji.

Zifuatazo ni baadhi ya picha zikionyesha mandhali ya miji na barabara, katika bonde hilo :
























* * * Lushoto Rise Up * * *

0 comments:

Post a Comment